Juzuu 1 Swala 4 MWF 2022-2023
UFAFANUZI WA NENO MUHIMU
- Kodi ya Mapato Jumla ya idadi ya mapato ambayo imepokelewa na mtu kwa mwaka wa fedha kutoka kwa ukodishaji/ liisi ya mali ambayo haiwezi kuhamisika kama shamba, nyumba (immovable property ) hapa Uganda ikikuwamu mapunguzo ya gharama ambayo yanahusika na mali hayo.
- Mwenye nyumba
Huu ni mtu yeyote ambaye anakodisha mali ambayo haiwezi kuhamishwa (immovable property) kwa mtu mwingine mkodishaji (Tenant) kwa thamani k.m malipo ya pesa. Mwenye nyumba anaweza kukuwa kama ni
• Mtu wa kibinafsi kama Mathew Etima
• Kampuni kama Kampuni RORA Ltd
• Shirika kama Property (U) Ltd
• Serikali, kama Wilaya ya Utawala ya Luwero. (Luwero District Administration)
•Taasisi kama Chuo Kikuu cha Makerere, UWESO.
• Taasisi ambayo imeoorodheshwa kama Benki ya Maendeleo ya Afrika (Africa Development Bank). C. Mkodishaji (Tenant)
Huu ni mtu ambaye anakodisha mali ya mtu mwingine kwa makubaliano ya kibiashara analipa thamani k.m pesa. Kodi ya ukodishaji inapewa mamlaka ya usanyaji, kutoka kwa kifungu cha S. 5 ya sheria ya kodi ya mapato. Hii kodi ya ukodishaji ambayo imepokelewa na mtu, inatozwa tafauti na kodi zingine.
KUHESABU KODI YA MAPATO YA UKODISHAJI. HATUA MUHIMU
Kwa mtu wa kawaida
Hatua 1: Amua jumla ya mapato ya ukodishaji kwa mwaka (R) kutoka kwa chanzo za mapato zote za mtu wa kibinafsi.
Hatua 11: Pumguza kiwango cha chini ambacho kinakubaliwa ya SH U 2, 820,000
Jua: Hakuna mapunguzo zingine ambazo zinakubaliwa. R – 2, 820, 000 = Mapato ambayo inafaa kutozwa
Hatua 111: Amua kodi ya mapato ya ukodishaji kwa cheo cha 12%
Kodi ambayo inafaa kulipwa ni = 12% X mapato ambayo inafaa kulipiwa kodi.
Kwa Washirika (Partnerships) kodi imepimwa kwa kila mshiriki kulingana na cheo cha kiwango ambacho amepekea.
Hatua1: Amua jumla ya kodi kwa mapato kwa mwaka (R) kwa kila msiriki (partner).
Hatua 11. Toa/punguza kiwango cha chini ambacho kinakubalika cha SH U 2,820,000.
Jua: Hakuna mapunguzo zingine ambazo zinakubalika.
Mapato ambayo inafaa kutozwa ni = R- 2,820,000
Hatua 111: Amua kodi ya ukodishaji kwa cheo cha 12% na zigawanye kulingana na mgawanyo wa msiriki (partnership stake).
Kwa Makampuni, Waminifu/matrasti (Trustees) Fedha ya kustaafu (retirement fund)
Hatua 1: Amua jumla ya kodi ya mapato ya ukodishaji (R) kutoka kwa chanzo zote za mapato
Hatua 11: Punguza hadi 50% ya jumla ya mapato ya Kampuni kama alowensiposho (allowance) ya matumizu/gharama na hasara R-50%R = Mapato ambayo inafaa kutozwa.
Jua yakwamba : gharama ambayo imedaiwa itafanyiwa thibitisho/ukaguzi ili kuzundua ukweli kupitia Shirika la Mamlaka ya Mapato Uganda, kwa hivyo gharama ambayo imetokea kwa operesheni na uzalishaji wa kodi ya ukodishaji pekee itakubaliwa.
Hatua 111: Amua kodi ya ukodishaji kwa cheo cha 30%. Kodi ambayo inafaa kulipwa ni = 30% X Mapato ambayo inafaa kutozwa.
KWA MFANO
A. Mtu wa kibinafsi
B. Namna inafaa kuhesabiwa: kama jumla ya mapato ni tuseme Sh 6,000,000 kwa mwaka, gharama ya huduma ya kliarensi (800,000) gharama ya urekebihshaji vitu (500,000) na riba (interest) kwa rehani/motigeji (800,000) hesabu kodi ya ukodishaji ambayo inafaa kulipwa.
Hatua 1: Amua jumla ya kodi ya mapato kutoka kwa chanzo za ukodishaji zote = Sh 6,000,000. Toa/punguza kwa kiwango cha chini ambacho kinakubalika cha SH U 2,820,000 = 6,000,000 – 2,820,000
Jua: Hakuna mapunguzo zingine ambazo zinakubalika. Kodi ambayo inafaa kutozwa ni = 3,180,000 Hatua 111: Hesabu kodi ya ukodishaji kwa cheo cha 12% = 12/100 X 3,180,000 Kodi ya ukodishaji ambayo inafaa kulipwa ni = SH U 381,600
- Ushirikiano (Partnerships) Ukitumia hesabu ya juu, kama Amos na Robert wako kwa Ushirikiano na migawo/ yao iko kwa uwiano (ratio) ya 2:3 halafu;
Mshiriki Amos = 2/5 X 381,600 = SH U 152,640
Mshiriki Robert = 3/5 X 381,600 = SH U 228,960
Kwa hivyo Mshiriki Amos atalipa SH U 152, 640 na Robert atalipa SH U 228,960
Kampuni
Kwa hali hii/Kwa mfano kama Kampuni kinapokea shilingi milioni 30, milioni 15 kilikuwa ndani chake ni ya ukodishaji wa mali. Gharama ya huduma usafirishaji vitu ni (3,000,000), askari wa ulinzi (4,000,000) na gharama ya marekebisho za vitu (4,000,000). Kodi ya ukodishaji ni kinahesabika kwa namna zifuatavyo;
Hatua 1: Amua jumla ya mapato zote kutoka kwa vyanzo vyote vya Kampuni = Sh U 15,000,000 Hatua 11: Punguza/Toa alowensi/posho ya gharama na hasara hadi 50%, ya jumla ya mapato ya ukodishaji kwa mwaka. Jumla ya gharama = 3,000,000 + 4,000,000 + 4,000,000 = 11,000,000 Kwa hivyo gharama ambayo inakubaliwa ya posho/ alowensi Posho/alowensi ambayo inakubaliwa ni = 50% X 15,000,000 = 7,500,000 Kodi ya ukodishaji ambayo inafaa kutozwa ni = 15,000,000 – 7,500,000 = 7,500,000
Hatua 111: Hesabu kodi ya mapato ya ukodishaji ni = 30% = 30/100 X 7,500,000 Kodi ya ukodishaji ambayo inafaa kulipwa ni = SHU 2, 250,000
JUKUMU YA MLIPAKODI
Weka/rejesha retani ya mapato ya ukodishaji wa mwaka wa mapato ukiambatisha (attaching) maandishi ya makubaliano kama uko nayo au risiti la ukodishaji ambayo imepewa wa/mkodishaji kwa muda ya mwaka
Tangaza vyanzo (sources) vya mapato vyote vya ukodishaji wa muda fulani ya mwaka ya mapato. Mwaka wa mapato inaanzia kwa tarehe 01 Mwezi wa Saba hadi tarehe 30 ya mwezi wa Sita au mwaka ambayo uliobadilishwa (substituted). Tuma/rejesha retani kwa kila mwaka kwa Shirika la Mamlaka ya Mapato Uganda, kupitia ofisi ya Mamlaka ya Mapato ambayo iko karibu nawe, kwa muda ya mwezi sita baada ya mwaka wa mapato kukamilika/ kuisha.
Lipa kodi ya mapato ya ukodishaji kwa tarehe yenyewe ambayo inakubaliwa kisheria
Mlipakodi anahaki ya kupokea mkopo/krediti ya kodi, kuhusiana na kodi ya ukodishaji yoyote ambayo imelipwa ya muda (provisional ) au kodi ambayo imelipwa mapema (advance tax ) kwa muda ya mwaka wa mapato. Hii inaweza kuhesabiwa kwa kodi ambayo ililipwa mapema kwa makubaliano (offset ) dhidi ya dhima (liability) kwa hivyo vyanzo vya kodi hutozwa tafauti